SW

24 (msimu wa 5)

Msimu wa Tano (pia unajulikana kama Siku ya 5) ya mfululizo wa kipindi cha televisheni cha 24 kilichoanza kurushwa hewani kuanzia tar. 15 Januari2006 na kumalizia msimu wake kunako tar. 22 Mei 2006.

Msimu wa 5 wa 24

Season 5 Cast
Nchi asilia Marekani
Mtandao Fox Broadcasting Company
Iko hewani tangu 15 Januari 2006 – 22 Mei 2006
Idadi ya sehemu 24
Tarehe ya kutolewa DVD 5 Desemba 2006
Msimu uliopita Msimu wa 4
Msimu ujao Msimu wa 6

Hadithi ya Msimu wa Tano inaanza na kushia 7:00 asubuhi. Muda wake uko sawa na ule wa msimu uliopita.

Dakika 10 za mwanzo zilikuwa zikipatikana kwenye DVD ya msimu uliopita.[1] Ilikuwa ikirushwa kwenye Sky One huko nchini Uingereza kabla ya kuanza rasmi kwa msimu wa tano.

. . . 24 (msimu wa 5) . . .

Msimu wa Tano (2006) ni seti ya miezi 18 baada ya Msimu wa Nne.

Baada ya matukio ya Msimu wa Nne, kachero wa CTU Jack Bauer sasa hivi anafanyakazi siku-hadi-siku akiwa kama mfanyakazi wa kampuni ya kusafisha mafuta akiwa chini ya jina la “Frank Flynn” mjini Mojave, California. Jack arejea zake nyumbani huko mjini kaskazini mwa mji wa Los Angeles kwa Diane Huxley, mama asiye na mume, na mtoto wake mwenye umri miaka 15 aliyeitwa Derek.

Msimu wa Tano ilitakiwa iwe siku kubwa katika kipindi cha urais cha Charles Logan. Amepanga kusaini mkataba wa muungano kupinga ugaidi na Rais wa Urusi Bw. Yuri Suvarov kwa hiari yake huko mjini Hidden Valley, California. Hii ni siku ambayo inaaminika kwamba iliendeshwa kinyume sana kuliko matukio ya siku zote, kama Mrusi gaidi aliyejitenga na serikali yake (imekihiswa kuwa Chechen, ingawa hili halijaelezwa vizuri) ambaye yeye ndiye aliyebeba mzigo mzima wa mashambulizi kwa imani ya kuwa mkataba ule utaumiza watu zao.

Baadaye, ikagundulika kwamba yale matukio yaliyotokea ni sehemu kubwa sana ya njama za kiserikali ya rais alioko madarakani Bw. Rais Charles Logan, Mkubwa wa Wafanyakazi Walt Cummings, mkandarasi wa Kitengo cha Ulinzi Christopher Henderson, kwa ushirikiano wa James Nathanson, na kundi la watu ambao hawajulikani wanaongoza na kushawishi matendo ya Logan watokao katika sehemu zisizojulikana, wakiongozwa na mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la “Graham” ambaye inawezekana ndiye aliyefanya mpango wa Jack kujifichua kutoka mafichoni, na matukio yote.

Mpango wao wa awali ulikuwa kuachia gesi ya neva juu ya magaidi wa Kirusi na kutumia msamaha huo kama maombi ya kuachia vikosi vya kijeshi vya kupinga mkataba wa ugaidi, na kumruhusu Logan kulinda maslahi ya petroli ya Kimarekani huko Asia ya Kati. Rais wa zamani David Palmer alianza kulijua hili na akauawa ili kumnyamazisha; kifo chake kimekuwa mhamasiko mkubwa kwa harakati za Jack (mbali ya kusingiziwa kumwua David Palmer). Kama jinsi alivyoeleza kwa mara kadhaa kwenye mzunguko wa siku, “Haya mambo binafsi.”

Hii ni orodha ya washiriki wakuu wa Msimu wa 5. Tazama Orodha ya wahusika wa 24 kwa orodha iliyokamili.

Manyota

Special Guest Stars

Wageni Maalumu Waliouza Sura

Wanaojirudia

. . . 24 (msimu wa 5) . . .

This article is issued from web site Wikipedia. The original article may be a bit shortened or modified. Some links may have been modified. The text is licensed under “Creative Commons – Attribution – Sharealike” [1] and some of the text can also be licensed under the terms of the “GNU Free Documentation License” [2]. Additional terms may apply for the media files. By using this site, you agree to our Legal pages . Web links: [1] [2]

. . . 24 (msimu wa 5) . . .

Back To Top