SW

Gaël Faye

Gaël Faye (alizaliwa Bujumbura, Burundi, 6 Agosti1982) ni rapa, mtunzi wa muziki, na mwandishiMfaransaMnyarwanda.

Gaël Faye

Maelezo ya awali
Amezaliwa (1982-08-06)6 Agosti 1982
Bujumbura, Burundi
Aina ya muziki Hip Hop
Kazi yake Rapa, mtunzi wa muziki, mwandishi

. . . Gaël Faye . . .

Gaël Faye alizaliwa mwaka wa 1982 mjini Bujumbura nchini Burundi. Mama yake ni mrwanda na baba yake ni mfaransa. Mama yake alikwenda kuishi Ufaransa lakini Gaël Faye alikaa Burundi na baba yake. Baada ya mwanzo wa Vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Burundi mwaka wa 1993 na Mauaji ya Kimbari ya Rwanda mwaka wa 1994, alikimbia nchi yake ya asili hadi nchini Ufarasa mwaka 1995. Alikuwa na umri wa miaka 13.[1][2] Alikua na mama yake wakati wa ujana mjini Versailles katika wilaya ya Yvelines nchini Ufaransa.[1] Alifurahishwa na muziki wa hip hop.[3]

Gaël Faye alisoma katika sekondari ya Jules-Ferry mjini Versailles, kisha katika shule ya biashara.[1][4] Halafu alipata shahada ya uzamili katika usimamizi wa fedha na alifanya kazi kwa miaka miwili katika kampuni ya kitegauchumi jijini London. Baadaye alitoka jijini kufanya uandishi na muziki.

Mwaka wa 2015, alihama na mke wake na binti zao wawili kuishi nchini Rwanda.

Gaël Faye na Edgar Sekloka waliunda bendi ya Milk Coffee and Sugar.[1] Walichapisha albamu ya kwanza mwaka wa 2009 na wameipa jina albamu hii Découverte du Printemps de Bourges mwaka wa 2011.[5]

Gaël Faye alichapisha albamu ya kwanza peke yake ambayo inaitwa Pili pili sur un croissant au beurre mwaka 2012. Albamu hii inasimulia tawasifu ya mwimbaji binafsi. Katika nyimbo Gaël Faye anahadithia kuhusu uhamisho, vita, Mauaji ya Kimbari ya Rwanda, na mapenzi.[5]

Gaël Faye alitoa tarehe 19 Oktoba 2018 wimbo wa Balade brésilliene na mwimbaji mbrazil Flavia Coelho.[6]

. . . Gaël Faye . . .

This article is issued from web site Wikipedia. The original article may be a bit shortened or modified. Some links may have been modified. The text is licensed under “Creative Commons – Attribution – Sharealike” [1] and some of the text can also be licensed under the terms of the “GNU Free Documentation License” [2]. Additional terms may apply for the media files. By using this site, you agree to our Legal pages . Web links: [1] [2]

. . . Gaël Faye . . .

Back To Top