SW

Kilimanjaro (Volkeno)

Kilimanjaro ni jina la mlima mrefu kuliko yote baraniAfrika. Mlima huo uko nchini Tanzania katika Mkoa wa Kilimanjaro. Una urefu wa mita 5,895 (futi 19,340).

Kilimanjaro mnamo 1911
Picha ya kwanza ya angani ya Kibo iliyochukuliwa na Walter Mittelholzer mnamo 1929
Tembo kwenye Hifadhi ya Kitaifa ya Amboseli dhidi ya Mlima Kilimanjaro
Mlima Kilimanjaro kama unavyoonekana kutoka manispaa ya Moshi katika Mkoa wa Kilimanjaro
mfano wa kilele cha mlima kilimanjaro
Mlima Kilimanjaro unavyoonekana kutoka Moshi
Kilele cha Kibo kwenye mlima Kilimanjaro

Hali halisi Kilimanjaro ni zaidi ya mlima tu, ni kama safu ndogo ya milima mitatu: Kibo, Mawenzi na Shira. Hiyo mitatu inaonekana kama vilele vitatu vya mlima mmoja, hivyo si vibaya kusema Kilimanjaro ni mlima.

Kijiolojia Kilimanjaro ni volkeno iliyolala kwa sasa. Kwenye kilele cha Kibogesi bado inatoka. Kumbukumbu ya wenyeji ina habari ya mlipuko mnamo mwaka1730.

Kilele cha juu cha Kibo kinaitwa Uhuru. Mtu wa kwanza kufika kileleni hapo alikuwa Johannes Kinyala Lauwo kutoka Marangu aliyewaongoza WajerumaniHans Meyer na Ludwig Purtschellertarehe6 Oktoba1889 wakati wa ukoloni wa Ujerumani. Wakati ule waliita ncha ya juu “Kaiser-Wilhelm-Spitze” (kwa Kijerumani: Kilele cha Kaisari Wilhelm) kwa heshima ya Kaisari wa Ujerumani.

Kibo ina theluji na barafuto ndogo kadhaa.

. . . Kilimanjaro (Volkeno) . . .

Ramani ya 1888 inayoonyesha jina “Kilima-Ndscharo” katika Afrika ya Mashariki ya Kijerumani.

Asili ya jina “Kilimanjaro” haijulikani kikamilifu. Vyanzo vya kimaandishi vinajulikana tangu takriban mwaka 1860 ambapo wapeleleziWazungu walitumia jina hilo katika taarifa zao wakidai “Kilimanjaro” ni jina la Kiswahili.[1] Pamoja na umbo hili kulikuwa pia na tahajia ya sehemu mbili ama “Kilima-Njaro”[2] au kwa namna ya Kijerumani “Kilima-Ndscharo”.

Johann Ludwig Krapf aliandika mnamo 1860 kuwa Waswahili kwenye pwani waliita mlima huo “Kilimanjaro”. Alisema pia ya kwamba hao Waswahili walieleza maana yake kuwa ama “mlima mkubwa” au “mlima wa misafara” ingawa mwenyewe hakukubali maelezo hayo. Kwa elezo la mwisho “Kilima” kilimaanisha “mlima” na “Jaro” labda “misafara”.[1]

Jim Thompson aliandika mnamo 1885 kuwa jina Kilima-Njaro lilichukuliwa mara nyingi kuwa na maana ya “mlima mkubwa” lakini mwenyewe alipendelea maelezo tofauti yaliyosema “mlima mweupe”. [3] “Njaro” ni Kiswahili cha Zamani kwa “ng’ara”.[4]

Vivyo hivyo Krapf aliandika ya kwamba aliwahi kuwatembela Wakamba mnamo 1849 walioita mlima “Kima jaJeu” yaani mlima mweupe [5] Leo hii Wakamba wangesema “Kiima Kyeu” na elezo hili limekubaliwa na watafiti mbalimbali.

Wengine huona ya kwamba ni Wazungu wasiojua Kiswahili vema waliochanganya “mlima” na “Kilima”.

Wengine wamejaribu kuona msingi wa jina katika lugha ya Kichagga. Hapo wanadai uwezekano kuwa “Kileman” limetokana na neno la Kichagga “kileme” linalomaanisha “kinachoshinda” au neno “kilelema” linalomaanisha “kilichokuwa vigumu, kilichoshindikana”. Katika hoja hiyo “Jaro” imetokana na Kichagga “njaare” (aina ya ndege, au kufuatana na wengine chui) au kutoka neno “jyaro” (msafara). Elezo lingine ni kwamba Wachagga walisema mlima huo hauwezi kupandwa “kilemanjaare” au “kilemajyaro” na wapagazi au wafasiri kutoka pwani waliichukua kuwa jina la mlima na kutafsiri vile kwa Wazungu.

Tangu miaka ya 1880 mlima umekuwa sehemu ya Afrika ya Mashariki ya Kijerumani ukaitwa “Kilima-Ndscharo” kwa Kijerumani.[6]

Tarehe 6 Oktoba1889Hans Meyer alikuwa mtu wa kwanza anayejulikana kupanda mlima na kufika hadi kilele cha Kibo. Alichagua jina la “Kaiser-Wilhelm-Spitze” (“Ncha ya Kaisari Wilhelm[7]).[8]

Jina hilo lilitumika hadi Tanzania ilipoundwa mwaka 1964,[9] na kilele kubadilishiwa jina kuwa “Uhuru”, likiwa na maana ya “Kilele cha Uhuru” [10]

. . . Kilimanjaro (Volkeno) . . .

This article is issued from web site Wikipedia. The original article may be a bit shortened or modified. Some links may have been modified. The text is licensed under “Creative Commons – Attribution – Sharealike” [1] and some of the text can also be licensed under the terms of the “GNU Free Documentation License” [2]. Additional terms may apply for the media files. By using this site, you agree to our Legal pages . Web links: [1] [2]

. . . Kilimanjaro (Volkeno) . . .

Back To Top