SW

Puju

Puju au puju pembe ni samaki wa baharini wa jenasiNaso katika familiaAcanthuridae wa odaPerciformes. Kama ndugu wao kangaja wana jozi za miiba kwa umbo la vijembe kwenye kila upande wa msingi wa mkia. Lakini rangi zao si kali kama zile za kangaja. Spishi fulani huitwa karanzaga au sange pia.

Puju

Puju madoadoa (Naso brevirostris)

Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Actinopterygii (Samaki walio na mapezi yenye tindi)
Oda: Perciformes (Samaki kama ngege)
Familia: Acanthuridae (Samaki walio na nasaba na kangaja)
Bonaparte, 1832
Jenasi: Naso
Lacépède, 1801
Spishi: Spishi 20:

 • N. annulatus(Quoy & Gaimard, 1825)
 • N. brachycentron)Valenciennes, 1835)
 • N. brevirostris(Cuvier, 1829)
 • N. caeruleacaudaRandall, 1994
 • N. casesiusRandall & Bell, 1992
 • N. elegans(Rüppell, 1829
 • N. fageniMorrow, 1954
 • N. hexacanthus(Bleeker, 1855)
 • N. lituratus(J.R. Forster, 1801)
 • N. lopeziHerre, 1927
 • N. maculatusRandall & Struhsaker, 1981
 • N. mcdadeiJ.W. Johnson, 2002
 • N. minor(J.L.B. Smith, 1966)
 • N. reticulatusRandall, 2001
 • N. tergusH.-C. Ho, K.-N. Shen & C.-W. Chang, 2011
 • N. thynnoides(Cuvier, 1829)
 • N. tonganus(Valenciennes, 1835)
 • N. tuberosusLacépède, 1801
 • N. unicornis(Forsskål, 1775)
 • N. vlamingii(Valenciennes, 1835)

. . . Puju . . .

Spishi kadhaa za puju zina kivimbe kirefu kwenye paji. Kwa wengine hufanana na kangaja lakini huwa ni wakubwa zaidi. Puju mkia-ncha-nyeupe anaweza kufika urefu wa m moja. Wana jozi moja, mbili au tatu za vijembe. Hula miani kwenye miamba ya matumbawe.

Puju hupendwa na wavuvi kwa mkuki na kwa kawaida hubanikwa wazima.

. . . Puju . . .

This article is issued from web site Wikipedia. The original article may be a bit shortened or modified. Some links may have been modified. The text is licensed under “Creative Commons – Attribution – Sharealike” [1] and some of the text can also be licensed under the terms of the “GNU Free Documentation License” [2]. Additional terms may apply for the media files. By using this site, you agree to our Legal pages . Web links: [1] [2]

. . . Puju . . .

Back To Top