SW

Simba walawatu wa Tsavo

Simba walawatu wa Tsavo walikuwa simba wawili waliojulikana sana kwa kuwala binadamu. Simba hawa walisababisha vifo vya idadi kubwa ya wajenzi wa Reli ya Kenya-Uganda, tangu Desemba, 1898.

Makala haina vyanzo vya kutosha

Makala (au sehemu ifuatayo ya makala) inatoa habari bila kuonyesha vyanzo au uthibitisho wowote. Ona namna ya kutaja vyanzo hapa:Wikipedia:Umaarufu na Kutaja vyanzo.
Ni lazima kuboresha makala kwa kutafuta vyanzo na kuvitaja kama marejeo. Bila masahihisho hayo sehemu za makala au yote inaweza ikafutwa.
Unaweza kuondoa kigezo hiki mara vyanzo sahihi vimeingizwa katika makala

Wala-Watu wa Tsavo katika maonyesho ya Uwanjani katika Musiamu ya Historia ya Kimaumbile jijini Chicago, Illinois.

. . . Simba walawatu wa Tsavo . . .

Mnamo Machi 1898, wakati wa ujenzi wa Reli ya Kenya-Uganda, mhandisi John Henry Patterson aliongoza ujenzi wa daraja juu ya Mto Tsavo nchini Kenya. Wakati wa ujenzi huu, wafanyikazi wengi wa India waliuawa na simba wawili wa kiume (Simba wa Tsavo), ambao walivamia watu hemani mwao na kuwararua. Wajenzi hawa walijenga maboma yenye kuta za miiba kuzunguka hema zao ili kuwaepuka wala-watu hawa; lakini simba hawa waliweza kujipenyeza. Patterson alijaribu mara kadhaa kuwawekea mitego na kuwafukuza usiku kutika mtini. Baaada ya majaribio mengi bila mafanikio, hatimaye alimpiga risasi mmoja wao mnamo 9 Desemba 1898. Wiki tatu baadaye, mnyama wa pili alipatikana na kuuawa. Idadi kamili ya watu waliouawa na wanyama hawa haijadhihirika. Wakati wa uhai wake, Patterson alitoa takwimu nyingi tofauti tofauti, moja ikikisia kwamba kulikuwa na waadhiriwa wengi, takribani 135.[1][2] Utafiti wa hivi maajuzi unaonyesha kwamba takwimu hizi zilikuwa takribani 35.

Patterson anaandika kuwa alimjeruhi simba wa kwanza akitumia risasi kutoka bunduki aina ya martini-Enfield .303. Risasi hii ilimpata katika miguu ya nyuma na akafanikiwa kutoroka. alirudi usiku akijaribu kumsaka Patterson hata alipojaribu kumwinda. patterson alimpiga risasi mara kadhaa akitumia bunduki ya .303 Lee Enfield, huku akimfuatilia keshoye na kumpata akiwa amefariki. Kwa ujumla, alimpiga risasi mara tano. Simba wa pili alipigwa risasi mara tano kwa kutumia bunduki ya .303 Lee Enfield, lakini bado aliweza kusimama na kujaribu kumsogelea kwa maumivu makali, ambapo alimpiga risasi mbili zaidi, moja katika kifua na ya pili kwa kichwa na akamuua. Anadai kuwa simba huyo alifariki huku akining’ini katika taga la mti lililoanguka, bado akijaribu kumfikia Patterson.[3]

Baada ya kutumika kwa miongo miwili na nusu kama matandiko ya Patterson, ngozi za simba hao ziliuzwa kwa Musiamu ya Uwanjani ya Chicago kwa jumla ya Dola za Marekani 5,000. Simba hao walifika kwa Musiamu katika hali mbaya. Walijengwa upya na sasa hivi wako katika maonyeshho ya kudumu pamoja na viwiliwili vyao. Simba waliopandikwa hapo wako na kipimo kidogo kuliko unene wa kutisha ambao Patterson anausimulia, pengine kwa kuwa Patterson alidanganya juu ya unene huo, au kwa sababu walikuwa wamepunguzwa ili kutumika kama matandiko ya Kombe nyumbani mwa Patterson.

Masimulizi ya Patterson yalichapishwa katika kitabu chake cha 1907, The Man-Eaters of Tsavo.

. . . Simba walawatu wa Tsavo . . .

This article is issued from web site Wikipedia. The original article may be a bit shortened or modified. Some links may have been modified. The text is licensed under “Creative Commons – Attribution – Sharealike” [1] and some of the text can also be licensed under the terms of the “GNU Free Documentation License” [2]. Additional terms may apply for the media files. By using this site, you agree to our Legal pages . Web links: [1] [2]

. . . Simba walawatu wa Tsavo . . .

Back To Top