.svg/langsw-800px-Flag_of_Venezuela_(state).svg.png)
Venezuela ni nchi kaskazini mwa Amerika ya Kusini.

Imepakana na Brazil, Guyana na Kolombia.
Mbele ya pwani ya Bahari ya Karibi kuna madola ya visiwani ya Aruba, Antili za Kiholanzi na Trinidad na Tobago.
Venezuela ilikuwa koloni la Hispania hadi mwaka 1811 na lugha ya Kihispania ni lugha ya kitaifa.
Kikatiba Venezuela ni shirikisho la jamhuri.
. . . Venezuela . . .
Jina la nchi ni umbo la Kihispania la jina la mji wa Venezia (Italia). Amerigo Vespucci, mpelelezi Mwitalia katika utumishi wa mfalme wa Hispania, aliona vijiji vya wenyeji waliojenga nyumba juu ya maboriti yaliyosimamishwa katikati ya maji karibu na mwambao pasipo kina. Vijiji vilimkubusha mji wa Venezia uliojengwa vilevile. Venezuela yamaanisha “Venezia Ndogo” katika Kihispania.
Venezuela ina eneo la km² 916,445 (kama Namibia) ikiwa na pwani yenye urefu wa km 2,800. Asilimia 39 za eneo hili ni misitu, mashamba ya kulimwa ni 4%, eneo la mifugo 20%, mazao ya kudumu kama kahawa 1%.
Kuna kanda nne za kijiografia:
- tambarare za pwani karibu na Maracaibo katika kaskazini-magharibi
- milima ya Andes
- tambarere za mto Orinoko katikati ya nchi
- nyanda za juu za Guayana katika kusini-mashariki
Nyanda za juu za Guayana zina milima ya pekee: kuna milima ya meza 115 inayoitwa “tepui” katika lugha ya wakazi asilia. Kiekolojia hilo ni eneo muhimu kwa sababu milima mingi ina mimea na wanyama wa pekee, tofauti na milima jirani, na inapatikana hapa tu kote duniani.
Maporomoko marefu duniani yatelemka kutoka milima hii kama vile maporomoko ya Salto del Angel (“anguko la malaika“) ambako maji huanguka mita 965.
. . . Venezuela . . .