SW

Historia ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo

Historia ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo inahusu eneo la Afrika ya Kati, hasa katika beseni ya mto Kongo, ambalo wakazi wake leo wanaunda Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

. . . Historia ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo . . .

Wakazi wa kwanza huaminiwa kuwa wawindaji wa jamii ya Wasani na ya Wabilikimo.

Katika karne za BK walifika wahamiaji Wabantu wenye ujuzi wa kilimo na uhunzi.

Jina la Kongo lahusiana na mto Kongo unaopitia nchi yote na pia Ufalme wa Kongo uliopatikana zamani katika sehemu za magharibi za Angola na Kongo ya leo.

Mnamo karne ya 15, wakati wapelelezi wa kwanza Wareno walipofika kwenye pwani za Afrika, milki kubwa katika nchi ya Kongo ya magharibi pamoja na Angola ya kaskazini ilikuwa Ufalme wa Kongo. Wakati wa uenezaji mkuu ufalme huu ulianza kwenye mwambao wa Atlantiki na kuendelea hadi mto Kwango kwenye mashariki, halafu maeneo kutoka Pointe-Noire (leo: Jamhuri ya Kongo, upande wa kaskazini ya Cabinda) upande wa kaskazini hadi mto Loje (leo: mji wa Ambriz) katika kusini.

Mtawala alikuwa na cheo cha Manikongo na ufalme uligawiwa kwa majimbo sita. Baada ya kufika kwa Wareno wafalme na matabaka ya juu walikuwa Wakristo. Ufalme uliporomoka kutokana na vita vilivyosababishwa na biashara ya watumwa na kuingilia kwa wafanyabiashara ya watumwa katika siasa ya ndani. Hata hivyo, nasaba za watawala waliotumia cheo cha “Awenekongo” waliendelea kukaa katika mji mkuu wa kale M’banza-Kongo (iliyobadilishwa jina kuitwa San Salvador) hadi mwaka 1914 ambako Wareno walifuta mabaki ya uhuru na kufanya eneo lililobaki sehemu kamili ya koloni lao la Angola.

Upande wa kusini, kuanzia karne ya 17, kulikuwa na ufalme ulioitwa Dola la Kazembe.

Picha za watoto waliokatwa mikono kama adhabu chini ya Leopold II zilienea na kusababisha madai ya kumwondolea utawala wa Kongo.

Nchi jinsi ilivyo ilianzishwa kama Dola huru la Kongo likiwa mali binafsi ya mfalmeLeopold II wa Ubelgiji. Historia yake ni ya aibu na ya ukatili kupindukia.

Utawala wa mfalme ulionekana kuwa wa kinyama na upinzani dhidi yake ulikua katika nchi nyingi za dunia.

Hatimaye alipaswa kukabidhi koloni lake binafsi mikononi mwa serikali ya Ubelgiji iliyomlipa fidia kwa mali aliyoacha.

Kati ya mwaka 1908 hadi 1960 ilikuwa koloni la Ubelgiji baada ya kuhamishiwa mikononi mwa serikali ya Ubelgiji.

Katika miaka 1925 hadi 1946 maeneo ya Rwanda na Burundi yalitawaliwa kama sehemu za Kongo ya Kibelgiji.

. . . Historia ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo . . .

This article is issued from web site Wikipedia. The original article may be a bit shortened or modified. Some links may have been modified. The text is licensed under “Creative Commons – Attribution – Sharealike” [1] and some of the text can also be licensed under the terms of the “GNU Free Documentation License” [2]. Additional terms may apply for the media files. By using this site, you agree to our Legal pages . Web links: [1] [2]

. . . Historia ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo . . .

Back To Top