SW

Kuwait

Kuwait (kwa Kiarabu: الكويت ‎) ni nchi ndogo ya Uarabuni kwenye Ghuba ya Uajemi.

دولة الكويت
Dawlat al Kuwayt

Kuwait
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa: (hakuna)
Wimbo wa taifa: watani alkuwait وطني الكويت سلمت للمجد
(Taifa langu la Kuwait)
Mji mkuu Jiji la Kuwait
29°22 N 47°58 E
Mji mkubwa nchini Salmiya
Lugha rasmi Kiarabu
Serikali

Emir
Waziri Mkuu
Ufalme wa kikatiba
Nawaf Al-Ahmad Al-Jaber Al-Sabah
Jaber Mubarak al-Sabah
Uhuru
kutoka Uingereza
19 Juni1961
Eneo
 – Jumla
 – Maji (%)
 
17,820 km² (ya 157)
Idadi ya watu
 2014 kadirio
 2005 sensa
 – Msongamano wa watu
 
4,044,500 2 (140)
2,213,403
200.2/km² (ya 68)
Fedha Kuwaiti Dinar (KWD)
Saa za eneo
 – Kiangazi (DST)
(UTC+3)
(UTC+3)
Intaneti TLD .kw
Kodi ya simu +965

Ramani ya Kuwait
Kuwait inavyoonekana kutoka angani (2001)
Jiji la Kuwait

Imepakana na Irak na Saudia.

. . . Kuwait . . .

Karibu nchi yote ni jangwa, lakini kuna pwani na visiwa vidogo.

Historia ya Kuwait ilianza kama utemi mdogo chini ya familia ya Al-Sabah iliyokuwa chini ya Sultani wa Uturuki aliyetawala nchi jirani ya Irak hadi vita kuu ya kwanza ya dunia.

Tangu kuingia kwa Waingereza katika nchi za ghuba, mwaka 1899watawala wa Kuwait walijiweka chini ya ulinzi wa Uingereza kwa sababu waliuona afadhali kuliko ukuu wa Uturuki.

Waingereza walitetea hali yake ya pekee dhidi ya Waosmani na baadaye dhidi ya Saudia.

Baada ya kuporomoka wa dola la Uturuki Kuwait iliendelea kama nchi lindwa chini ya Uingereza hadi kupata uhuru wake tarehe 19 Juni1961.

Katika miaka iliyofuata Kuwait iliona madai ya Irak ya kuwa tangu zamani Kuwait ni mkoa wake uliotengwa na ukoloni.

Tarehe 2 Agosti1990dikteta wa IrakSaddam Hussein alivamia Kuwait na kuiteka. Katika vita ya pili ya ghuba Marekani pamoja na nchi nyingine ilishambulia jeshi la Irak katika Kuwait na kurudisha serikali ya Emir al Sabah.

Kati ya wakazi 4,044,500 asilimia 30 pekee ni wananchi au Wakuwait wenyewe. Wengine wote ni watu waliokuja kufanya kazi na kuishi hapo. Pamoja na wahamiaji kutoka nchi jirani, 60% ya wakazi ni Waarabu. Zaidi ya 30% tena wana asili ya India au nchi nyingine za Asia. Waafrika ni 76,698.

Lugha rasmi ni Kiarabu; wananchi wanakiongea kwa lahaja maalumu. Kiingereza pia kinatumika hasa, hasa katika biashara.

Upande wa dini, wananchi karibu wote ni Waislamu, hasa Wasuni (70%), lakini pia Washia (30%). Ndiyo dini rasmi. Wakristo ni zaidi ya 10%, lakini karibu wote ni wahamiaji. Wahindu kutoka India ni wengi zaidi kidogo (karibu 15%). Wabuddha ni 2%.

Nchi ni tajiri kutokana na wingi wa mafuta ya petroli yaliyopo chini ya ardhi yake. Akiba zake ni kama 10% za akiba za dunia yote. Kabla ya kupatikana kwa mafuta mwaka 1938 nchi ilikuwa maskini lakini sasa ni kati ya nchi tajiri zaidi duniani.

Kabla ya kugunduliwa kwa mafuta palikuwa na kilimo kidogo sana, halafu ufugaji na hasa uvuvibaharini.

. . . Kuwait . . .

This article is issued from web site Wikipedia. The original article may be a bit shortened or modified. Some links may have been modified. The text is licensed under “Creative Commons – Attribution – Sharealike” [1] and some of the text can also be licensed under the terms of the “GNU Free Documentation License” [2]. Additional terms may apply for the media files. By using this site, you agree to our Legal pages . Web links: [1] [2]

. . . Kuwait . . .

Back To Top