SW

Maadili ya kiutu

article - Maadili ya kiutu

Maadili ya kiutu ni yale yanayotakiwa kupatikana katika binadamu yeyote ili aweze kutenda kwa uadilifu kadiri ya utu wake unaomtofautisha na wanyama, yaani hasa akili inayomwezesha kufikiria na kuelewa maana na matokeo ya matendo yake.

Maadili yakipambana na vilema, vioo vya rangi vya karne ya 14 katika Niederhaslach Church.

Maadili bawaba

Kadiri ya wanafalsafa wa Ugiriki wa kalePlato na Aristotle, maadili hayo ni mengi (si chini ya 40), lakini yanategemea manne (maadili bawaba): busara, haki, nguvu na kiasi.

. . . Maadili ya kiutu . . .

Katika Biblia, upendo unadai pamoja na imani na tumaini (maadili ya Kimungu), maadili ya kiutu, ambayo yote yanategemea manne ya msingi: busara, haki, nguvu na kiasi. “Huwafundisha watu kiasi, na ufahamu, na haki, na ushujaa; wala hakuna mambo ya kuwafaa zaidi kwa maisha” (Hek 8:7).

Maadili ya kiutu yanapatikana na kukua kwa juhudi za kutenda mema hadi kuzoea na kupata msimamo. Katika kufanya hivyo tunasaidiwa na neema ya Mungu. “Uweza wake wa Uungu umetukirimia vitu vyote vipasavyo uzima na utauwa… mkijitahidi sana kwa upande wenu, katika imani yenu tieni na wema, na katika wema wenu maarifa, na katika maarifa yenu kiasi, na katika kiasi chenu saburi, na katika saburi yenu utauwa, na katika utauwa wenu upendano wa ndugu, na katika upendano wa ndugu, upendo. Maana mambo hayo yakiwa kwenu na kujaa tele, yawafanya ninyi kuwa si wavivu wala si watu wasio na matunda, kwa kumjua Bwana wetu Yesu Kristo” (2Pet 1:3,5-8).

Tunahitaji busara kwa sababu ndiyo adili linalotakiwa kuongoza utekelezaji wa mengine yote, kwa kuzingatia kila mara yaliyo mema kweli kwetu na kuchagua namna inayofaa kuyafikia. “Iweni na busara kama nyoka, na kuwa watu wapole kama hua” (Math 10:16). “Wale wenye busara walitwaa mafuta katika vyombo vyao pamoja na taa zao” (Math 25:4). “Maana ni nani katika ninyi, kama akitaka kujenga mnara, asiyeketi kwanza na kuhesabu gharama, kwamba anavyo vya kuumalizia? Asije akashindwa kuumaliza baada ya kuupiga msingi, watu wote waonao wakaanza kumdhihaki, wakisema, ‘Mtu huyu alianza kujenga, akawa hana nguvu za kumaliza’” (Lk 14:28-30).

Tunahitaji haki kwa sababu ndiyo msimamo wa kumpatia kila mmoja kile anachostahili. “Mwenye kanzu mbili na ampe asiye na kanzu; na mwenye vyakula afanye vivyo hivyo… Msidhulumu mtu, wala msishitaki kwa uongo; tena mtoshewe na mshahara wenu” (Lk 3:11,14). “Mpeni Kaisari yaliyo ya Kaisari, na yaliyo ya Mungu mpeni Mungu” (Mk 12:17).

Tunahitaji nguvu kwa sababu ndiyo msimamo wa kutorudi nyuma mbele ya ugumu wa kutenda mema yanayotupasa. “Mwenye kuvumilia hata mwisho, ndiye atakayeokoka” (Math 24:13).

Tunahitaji kiasi kwa sababu ndio msimamo wa kutumia vitu kadiri inayotufaa tu. Hasa ni muhimu kuwa na kiasi katika masuala ya jinsia. “Usizini. Wala usiibe… Wala usimtamani mke wa jirani yako… wala kitu chochote alicho nacho jirani yako” (Kumb 5:18-19,21). “Ikimbieni zinaa. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe” (1Kor 6:18).

Kati ya maadili mengine, Yesu alihimiza hasa upole na unyenyekevu, yanayotulinganisha naye kwa namna ya pekee. “Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu, kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo, nanyi mtapata raha nafsini mwenu” (Math 11:29). “Mtu anayetaka kuwa mkubwa kwenu, atakuwa mtumishi wenu, na mtu anayetaka kuwa wa kwanza wenu, atakuwa mtumwa wa wote. Kwa maana Mwana wa Adamu naye hakuja kutumikiwa, bali kutumika, na kutoa nafsi yake iwe fidia ya wengi” (Mk 10:43-45).

. . . Maadili ya kiutu . . .

This article is issued from web site Wikipedia. The original article may be a bit shortened or modified. Some links may have been modified. The text is licensed under “Creative Commons – Attribution – Sharealike” [1] and some of the text can also be licensed under the terms of the “GNU Free Documentation License” [2]. Additional terms may apply for the media files. By using this site, you agree to our Legal pages . Web links: [1] [2]

. . . Maadili ya kiutu . . .

Back To Top