SW

Pesa

Pesa ni chombo cha kubadilishana bidhaa na huduma kati ya watu. Pesa yenyewe haina faida, haitoshelezi mahitaji ya binadamu ila imekubalika katika jamii kama njia ya kujipatia mahitaji mengine.

Pesa za Afrika ya Mashariki
Pesa ya Euro

Kuna maneno mengine ya Kiswahili kwa pesa kama vile hela, fedha au sarafu.

Mfumo wa sarafu unamaanisha utaratibu wa kutoa na kusimamia pesa katika uchumi wa kisasa.

. . . Pesa . . .

Sarafu ya mwaka 640 KK kutoka Lydia

Kiasili watu walibadilishana vitu kwa mfano ng’ombe mmoja kwa mbuzi kadhaa au mazao kwa samaki n.k.

Baadaye imeonekana ya kwamba itasaidia zaidi kama kiwango fulani inapatikana kwa vitu vyote.

Metali zilizokuwa haba zilitumiwa kama kipimo hiki, kwa mfano dhahabu, fedha au shaba. Vilipimwa kufuatana na uzito.

Hatua iliyofuata ilikuwa kutumia vipande vya metali hizi vilivyogongwa mihuri halafu hapakuwa na lazima ya kuvipima kimoja-kimoja. Inavyojulikana Wachina walikuwa watu wa kwanza waliochukua hatua hii katika milenia ya 2 KK. Hii ilikuwa mwanzo wa sarafu.

Pesa hutolewa na serikali ya nchi au na taasisi kama benki kuu inayofanya kazi hii kwa niaba ya serikali. Mwanzoni sarafu ilikuwa sawa na kiasi fulani cha dhahabu au fedha.

Hatua nyingine ilikuwa kutolewa kwa pesa ya karatasi au benknoti zilizoahidi kumpatia mtu yeyote kiasi kilichoandikwa kwa dhahabu au fedha yenyewe. Kwa muda mrefu benki kuu zilikuwa na hazina ya dhahabu iliyolingana na kiasi cha benknoti zilizochapishwa.

Tangu mwisho wa karne ya 20 nchi kadhaa zilianza kutoa benknoti za plastiki kwa sababu zinadumu kushinda noti za karatasi, tena ni vigumu zaidi kwa wajanja kutengeneza pesa bandia.

Katika karne ya 20 nchi zote zilifanya hatua ya kuacha makadirio ya dhahabu kwa sababu thamani ya bidhaa katika jamii ilipita kiasi cha dhahabu iliyopatikana. Siku hizi jumla ya pesa inayotolewa inatakiwa kulingana na thamani ya rasilmali ya taifa fulani.

Pale ambako serikali inachapisha benknoti kushinda kiwango hicho, thamani ya pesa inashuka na mfumko wa bei unatokea.

Pesa 1 ya Afrika ya Mashariki ya Kijerumani (hadi 1904) – nyuma; maandishi yasema: “Deutsch-Ostafrikanische Gesellschaft 1892″
Pesa 1 ya Afrika ya Mashariki ya Kijerumani (hadi 1904) – mbele; maandishi yasema: “sharaka almaniya 1309”

. . . Pesa . . .

This article is issued from web site Wikipedia. The original article may be a bit shortened or modified. Some links may have been modified. The text is licensed under “Creative Commons – Attribution – Sharealike” [1] and some of the text can also be licensed under the terms of the “GNU Free Documentation License” [2]. Additional terms may apply for the media files. By using this site, you agree to our Legal pages . Web links: [1] [2]

. . . Pesa . . .

Back To Top