SW

Uislamu

Uislamu (kwa Kiarabu: الإسلام al-islam) ni dini inayotokana na mafunzo ya MtumeMuhammad.

Kaaba ni kibla ya Waislamu wote duniani wakati wa swala.

Wafuasi wa imani hiyo huitwa “Waislamu” na wanakadiriwa kuwa milioni 1,800 hivi. Hivyo ni dini ya pili duniani yenye wafuasi wengi baada ya Ukristo wenye wafuasi milioni 2,400.

Uislamu ni ile imani kuwa muumba ni mmoja tu kwa dhati na sifa zake. Nguzo nyingine za imani zinajengwa juu ya imani ya Mungu mmoja wa kweli, imani juu ya maisha baada ya kifo, imani juu ya Malaika wa Mungu, vitabu vyake na kudra na tafsiri ya vitendo ya imani hii ni: Sala, Zakah, Saumu na Hija.

Sehemu ya mfululizo wa makala juu ya

Uislamu

Imani na ibada zake

Umoja wa Mungu
Manabii
Misahafu
Malaika
Uteule
Kiyama
Nguzo za Kiislamu
ShahadaSwalaSaumu
HijaZaka

Waislamu muhimu

Muhammad

Abu BakrAli
Ukoo wa Muhammad
Maswahaba wa Muhammad
Mitume na Manabii katika Uislamu

Maandiko na Sheria

Qur’anSunnahHadithihttps://sw.wikipedia.org/w/index.php?search=Ali%20ibn%20Abu%20Talib&title=Maalum%3ATafuta&wprov=acrw1_2
Wasifu wa Muhammad
Sharia
Elimu ya Sheria za KiislamuKalam

Historia ya Uislamu

Historia
SunniShi’aKharijiyaRashidunUkhalifaMaimamu

Tamaduni za Kiislamu

ShuleMadrasa
TauhidiFalsafaMaadili
Sayansi
SanaaUjenziMiji
KalendaSikukuu
Wanawake
ViongoziSiasa
Uchumi
UmmaItikadi mpyaSufii

Tazama pia

Uislamu na dini nyingine
Hofu ya Uislamu

. . . Uislamu . . .

Imani katika Uislamu ni kumwamini Mungu mmoja tu peke yake anayeitwa Allah, ambaye hajazaa wala hajazaliwa na hafanani na yeyote yule. Kitabu kitakatifu cha Waislam ni Qur’an ambayo inaaminiwa ilifunuliwa kwa Mtume Muhammad kutoka kwa Mwenyezi Mungu mbinguni kupitia malaikaJibrili; ni kawaida kusema Qurani “iliteremshwa” kwa Muhammad. Kwa imani hiyo, kabla yake walioteremshiwa kitabu ni Musa (Torati), Daudi (Zaburi) na Isa (Injili).

Pamoja na Qurani kuna mafundisho ya Sunna na Hadith ambayo ni maneno ya mtume Muhammad na masimulizi juu ya matendo yake ambayo pengine hutazamiwa kama mwongozo katika Uislamu.

Allah ndiye Mungu pekee na muumba wa kila kitu. Qurani inasisitiza kwamba hana mshirika, hana baba wala mwana, hakuzaa wala hakuzaliwa, na hana mwanzo wala mwisho.

Pamoja na amri mbalimbali kuna mfumo wa sheria za kidini zinazoitwa kwa jumla “sharia“; inajumlisha maagizo kuhusu mambo mengi ya maisha ya kila siku, uchumi na siasa.

Muhammad alizaliwa mnamo mwaka 570BK kama mtoto wa mfanyabiashara mjini Maka uliopo kwenye Bara Arabu.

Kufuatana na mapokeo ya Kiislamu malaika Jibril alimtokea alipokuwa na umri wa miaka 40 yaani mnamo mwaka 610. Kutoka kwa malaika alipokea maneno ya Kurani na ufunuo huu uliendelea hadi mwisho wa maisha yake.

Mtume alitangaza yale aliyosikia kwa wafuasi wake na maneno haya yalianza kukusanywa tayari wakati wa maisha ya mtume. Baada ya kifo chake mwaka 632 khalifa wa tatu Uthman ibn Affan alikusanya muswada na kumbukumbu zote na kuziweka pamoja na kuwa kitabu kamili.

Ujumbe uliohubiriwa na Muhammad huko Maka ulipata wasikilizaji wachache, lakini viongozi wengi wa Kikuraishi, waliokuwa kabila kubwa Maka, waliwaona kama hatari kwa Maka na mwaka 622 Waislamu walipaswa kutoka Maka wakahamia Yathrib mji wa jirani uliojulikana baadaye kama Madina.

Uhamisho huu unaitwa hijra na tangu khalifa wa pili Umar ibn al-Khattab huhesabiwa kuwa ni chanzo cha kalenda ya Kiislamu.

Mjini Yathrib mtume aliendelea kuwa kiongozi wa kisiasa na wa kijeshi. Alifanya mapatano na watu wa Yathrib iliyoitwa baadaye “madinat an-nabi”” ikajulikana kwa kifupi kama Madina.

Kutoka Madina mtume alianza kushambulia misafara ya watu wa Maka akawashinda mara kadhaa. Wakati huohuo aliwafukuza Wayahudi wa Yathrib.

Mwaka 628 viongozi wa Maka walilazimishwa kufanya mapatano na Waislamu na mwaka 630 jeshi la Waislamu liliingia mjini Maka.

Mtume alipoaga dunia mwaka 632 sehemu kubwa ya Bara Arabu ilikuwa chini ya Uislamu tayari.

. . . Uislamu . . .

This article is issued from web site Wikipedia. The original article may be a bit shortened or modified. Some links may have been modified. The text is licensed under “Creative Commons – Attribution – Sharealike” [1] and some of the text can also be licensed under the terms of the “GNU Free Documentation License” [2]. Additional terms may apply for the media files. By using this site, you agree to our Legal pages . Web links: [1] [2]

. . . Uislamu . . .

Back To Top