SW

Uzbekistan

Uzbekistan ni jamhuri ya Asia ya Kati.

O‘zbekiston Respublikasi
O‘zbekiston Jumhuriyati
Ўзбекистон Республикаси

Jamhuri ya Uzbekistan
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa: —
Wimbo wa taifa: Wimbo la Taifa
Mji mkuu Tashkent
41°16 N 69°13 E
Mji mkubwa nchini Tashkent
Lugha rasmi Kiuzbeki
Serikali

Jamhuri
Shavkat Mirziyoyev
Abdulla Aripov
Uhuru

Ilitangazwa
Formation
Recognized
Completed

1747 kama Dola la Bukhara,
Dola la Kokand, Khwarezm
1 Septemba1991
8 Desemba1991
25 Desemba1991
Eneo
 – Jumla
 – Maji (%)
 
448,978 km² (ya 56)
4.9
Idadi ya watu
 Julai 2019 kadirio
 – Msongamano wa watu
 
32,768,725 (ya 41)
74.1/km² (ya 132)
Fedha Som ya Uzbekistan (UZS)
Saa za eneo
 – Kiangazi (DST)
UZT (UTC+5)
not observed (UTC+5)
Intaneti TLD .uz
Kodi ya simu +998

Imepakana na Afghanistan, Kazakhstan, Kyrgyzstan, Tajikistan na Turkmenistan.

Mji mkuu na pia mji mkubwa ni Tashkent.

Madrasa ya “Sherdor” mjini Samarkand

. . . Uzbekistan . . .

Uzbekistan ni nchi yenye historia ndefu. Ferghana, Tashkent, Bukhara, Khwarezm na Samarkand zilikuwa vitovu vya utamaduni wa binadamu tangu milenia ya 2 KK.

Katika karne kabla na baada ya Kristo eneo lilijulikana kama Sogdiana na Baktria. Miji yake ilikuwa na utajiri kutokana na biashara ya misafara kwenye barabara ya hariri kati ya China na Mashariki ya Kati.

Baadaye ilitawaliwa na milki mbalimbali za nje kama Uajemi.

Kuanzia uenezi wa Uislamu watu ba Uzbekistan waligeukia dini hiyo mpya.

Katika karne ya 14jemadariTimur alijenga milki kubwa na kuharibu nchi za magharibi hadi Uturuki. Alipamba mji mkuu wake Samarkand kwa majengo mazuri.

Baada ya Timur milki yake iliporomoka na Uzbekistan ilitawaliwa na madola mbalimbali ya kieneo yaliyokuwa hasa eneo la mji muhimu.

Katika karne ya 19Urusi ulieneza athira yake kuelekea kusini na kuunganisha madola ya Uzbekistan na milki yake.

Baada ya mapinduzi ya Urusi ya mwaka 1917 Uzbekistan ikawa sehemu ya Umoja wa Kisovyeti hadi kuporomoka kwake mwaka 1991. Ilijulikana kwa jina la “Jamhuri ya Kisovyeti ya Kijamii ya Kiuzbeki” hadi 1991.

Tarehe 31 Agosti 1991 ilijitangaza huru na kudai kufuata demokrasia na kuelekea soko huria, lakini hadi sasa haki za binadamu haziheshimiwi sana.

. . . Uzbekistan . . .

This article is issued from web site Wikipedia. The original article may be a bit shortened or modified. Some links may have been modified. The text is licensed under “Creative Commons – Attribution – Sharealike” [1] and some of the text can also be licensed under the terms of the “GNU Free Documentation License” [2]. Additional terms may apply for the media files. By using this site, you agree to our Legal pages . Web links: [1] [2]

. . . Uzbekistan . . .

Back To Top